Kamati  ya rufaa ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemfutia adhabu ya kufungiwa miaka kipa wa Simba, Denis Dioniz Richard.

Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Wakili Levocatus Kuuli amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba, Dennis aliyeadhibiwa wakati anacheza kwa mkopo Geita Gold ya Daraja la Kwanza, amfutiwa adhabu kwa sababu hakuna ushahidi wa kutosha dhidi yake.

Wakili Kuuli amesema walipitia rufaa za washitakiwa nane kati ya 22 waliotiwa hatuani kwa upangaji matokeo ya mechi za Daraja la Kwanza.

“Denis Dioniz Richard, kipa wa Geita ameachiwa huru kutokana na mapungufu yalikuwepo katika vifungu vya sheria za TFF,”amesema Wakili Kuulu.

Denis Dioniz Richard

Katika huku nyingine, Kocha msaidizi wa Geita, Abeid Choki ataendelea na kifungo chake cha kutojihusisha na mpira maisha baada ya rufaa yake kugonga mwamba.

Geita Gold Mining wataendelea na adhabu ya kushushwa daraja baada ya kubadilisha vithibitisho katika rufaa yao.
Kamisaa Salehe Mang’ola ataendelea na kifungo chake cha kutojihusisha na mpira maisha baada ya rufaa yake kugonga mwamba.

Katibu wa Chama cha Soka Tabora (TAREFA), Fate Remtulah, taendelea na kifungo cha kutojihusisha na mpira maisha baada rufaa yake kushindikana.

Mwenyekiti wa TAREFA, Yusuph Kitumbo ataendelea kutumikia kifungo cha kutojihusisha na mpira maisha a ya rufaa yake kugonga mwamba.

Polisi Tabora itaendelea kutumikia adhabu ya kushushwa daraja kutokana na rufaa yao kutupiliwa mbali, wakati JKT Oljoro adhabu yake ya kushushwa daraja itaendelea, bali watarudishiwa fedha yao ya rufaa shilingi milioni moja kutokana na kanuni kuwa na mapungufu.

Kamati hiyo imetoa siku 10 kuanzia leo kwa warufani kukata rufaa endapo hawakuridhika na hukumu hiyo.

Sumaye aishangaa Serikali ya Magufuli, adai Mwenendo wake ni hatari
David de Gea Na Chris Smalling Wang'ara Tuzo Za Man Utd

Comments

comments