Hatimaye Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amezungumzia suala la ndoa ya mama watoto wake, Zamaradi Mketema.

Ruge amezungumzia suala hilo ikiwa ni wiki kadhaa tangu isambae sauti iliyoaminika kuwa ni ya kwake, akisika mtu anazungumza na Zamaradi kwenye simu huku akilia kwa sauti ya mateso akilalama kuachwa.

Amesema kuwa kama mwanaume muungwana, huwa hazungumzii masuala ya ndani ya mahusiano yake ya kimapenzi, akitumia msemo wa kiingereza kuwa ‘Gentlemen don’t kiss and tell’, kwa tafrisi isiyo rasmi ‘hatubusi na kusimilia’. Msemo huu una maana ya kuwa wanandani hawasimulii kuhusu yao ya ndani.

Ruge amesema kuwa alikuwa anafahamu kila kilichokuwa kinaendelea kuhusu ndoa ya Zamaradi na kwamba alikuwa amempa baraka zote tofauti na ilivyokuwa ikizungumzwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa ameshtukizwa na kuumizwa.

“Kila kilichofanyika nilikuwa na taarifa na kilikuwa na baraka zangu. Ni sehemu ya maisha tunapitia. Kubwa kuliko yote, nina watoto wawili ambao nimezaa na Zamaradi. Nina mheshimu mno na hadi sasa naendelea kumheshimu mno,” Ruge amefunguka kupitia kipindi cha Clouds 360.

“Unajua kama kuna kitu nitakufundisha [mtangazaji] kama mdogo wangu , ‘When you are a gentleman, you don’t kiss and tell’ (Ukiwa mwanaume muungwana, haubusi na kusimulia). Vitu vingine vinabaki kuwa vyako binafsi vya ndani,” aliongeza.

Ruge ameeleza kuwa hata wikendi iliyopita alikuwa na watoto wake aliozaa na Zamaradi na kwamba anawapenda sana na hataacha kumheshimu mama yao.

Amesema amelazimika kulizungumzia hilo ili kuweka kumbukumbu sawa na sio vinginevyo.

Zamaradi alikuwa mtangazaji wa kipindi cha Take One cha Clouds TV. Alikifanya kipindi hicho kuwa maarufu huku akishiriki kuandaa filamu zilizoshika mitaa ikiwemo filamu ya ‘Kigodolo’.

JPM awatumia ujumbe Nape na Bashe kwa walichosema Bungeni
CUF yamshukia Mbowe kuhusu Prof. Lipumba