Leo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mfanyabiashara, James Rugemarila anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha amewataja Standard Chartered Tanzania Ltd na Standard Chartered Hong Kong kuwa ndiyo wezi wa fedha za Escrow.

Wezi hao amewataja mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Leornad Swai kueleza upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba iahirishwe hadi tarehe nyingine.

“Mwizi ni Standard Chartered Tanzania Ltd na Standard Chartered Hong Kong ambao wameisababishia serikali hasara ya Trilioni 37, pia nimewapelekea Takukuru washiriki wengine wa fedha hizo, hivyo ninaomba niendelee kuwa hai ili nije kuwa shahidi mzuri wa upande wa mashtaka kuhusu wezi hao.” ames Rugemarila

Pia Rugemarila amedai kuwa wezi hao ndio wamemuibia hata kwenye kampuni anayoisimamia ya VIP ambayo inawadai Trillion 16. Wakili Swai alidai kuwa ni kweli Rugemarila aliwasilisha taarifa ofisini kwao na wanazifanyia kazi kisha watatoa majibu.

Aidha Rugemarila ameiomba mahakama imkubalie akafanyiwe uchunguzi nchini India kwani anasumbuliwa na ugonjwa wa saratani kwa miaka 9 sasa huku mshtakiwa mwingine ambaye ni mmiliki wa IPTL Harbinder Singh Sethi ameiambia Mahakama kuwa tatizo lake la ugonjwa linajulikana.

Kutokana na hatua, Hakimu Simba amesema afya za washtakiwa ni muhimu hivyo wafanyiwe uchunguzi, pia anautaka upande wa mashtaka ukamilishe upelelezi kwa wakati, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi January 19,2018.

 

Video: Lissu adai alishambuliwa kisiasa
Video: Kangi Lugola afunguka kuhusu mke wake