Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu imemruhusu mfanyabiashara James Rugemarila kuwasilisha hoja zake za kutaka aachiwe huru.

Maombi hayo ameyawasilisha mstakiwa huyo leo Februari 27,2020 wakati shauri hilo lilipoitwa mahakamani hapo kwaajili ya kutajwa.

Rugemarila ni mkurugenzi wa VIP, na alikuwa mmiliki mwenza wa IPTL na wenzake wawili wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi .

Wastakiwa hao wa wameendelea kusota rumande toka mwaka 2017 kwa kesi ya kutakatisha fedha na kuisababishia Serikali hasara ya dola za kimarekani 22,198,544.60 na sh 309,461,300,158.27.

katibu wa CCM mbaroni kwa kumpachika mimba mwanafunzi
Nzige wavamia DRC