Serikali imesema ni ruksa kwa askari wa usalama barabarani kupiga picha kwa kujificha na kuituma kwa askari walio mbele ili kuweza kumkamata dareva aliyezidisha mwendo.

Hayo yamebainishwa jana Bungeni na wizara ya mambo ya Ndani ya nchi wakati akijibu swali la Mbunge wa Jang’ombe (CCM) Ali Hassan King.

king katika swali lake aliuliza kama ni sahihi kwa askari wa usalama barabarani kupigapicha magari yenye mwendokasi eneo moja kwa kificho na askari mwingine kukamata magari hayo eneo tofauti na tukio.

Katika majibu juu ya swali hilo, imeelezwa kuwa jeshi la polisi hutumia mbinu mbalimbali ili kubaini tabia za madereva wawapo barabarani na uhiari wa kutii sheria za barabarani.

Wizara hiyo imesema kupigapicha gari iliyozidisha mwendo katika eneo moja tena ambalo askari huwa amejificha ni mojawapo ya mbinu za kuhakikisha madereva wanatii sheria bila shuruti.

Mwakyembe: Roma hajatoroka nchini, corona imemkwamisha
DC Mjema afunguka wagonjwa wa Corona kutoroka Amana