Sheria inayokataza kuwafukuza wanafunzi wanaopata ujauzito shule imepitishwa na Bunge la Zimbabwe, ambapo watetezi wa haki za wanawake wamesema ni ushindi kwa harakati zao.

Sheria hiyo ambayo ilianza kutekelezwa mwaka 1999 imepitishwa wakati ambao shule na vyuo nchini humo vimefungwa ili kuthibiti maambukizi ya Covid 19.

Lakini, wazazi wa wanafunzi ambao wamepata ujauzito, wanafunzi wenyewe pamoja na uongozi wa shule husika hawaoni umuhimu kwa watoto wenye hali hiyo kurejea shuleni.

Mwaka 2018 asilimia kumi na mbili ya wanafunzi 57,000 nchini Zimbabwe waliacha masomo kutokana na kupata ujauzito na kuolewa.

CCM kupuliza kipyenga leo
Jeshi la zimamoto latoa tahadhari