Serikali imepanga kufanya marekebisho ya sheria ya usalama barabarani ili kuwaadhibu madereva wanaotumia simu wakati wanaendesha gari.

Uamuzi huo unatokana na kuwepo kwa matukio ya ajali ambayo yanahusishwa na madereva kupunguza umakini kwa kutumia simu wakati wanaendesha gari.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba alipokuwa akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/19.

Alisema kuwa mbali na kufanya marekebisho ya Sheria hiyo, watafanya uboreshaji wa Baraza la Taifa la Usalama wa Barabarani ili kulifanya kuwa taasisi kiongozi wa usalama barabarani.

Dkt. Mwigulu pia alisema kuwa wanakusudia kuondoa nukta kwenye leseni za madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani.

Aidha, alisema kuwa hali ya usalama barabarani imeboreka na ajali zimepungua kwa asilimia 35 kulinganisha na mwaka ulipopita.

“Takwimu zinaonesha kupungua kwa ajali barabarani kwa silimai 35.7 ilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2016/17,” alisema.

Ajali zinazotokana na madereva kutumia simu ni tatizo linaloikumba dunia ya sasa hali iliyosababisha baadhi ya nchi kuanzisha kampeni mbalimbali kuepusha janga hilo.

Video: Serikali yakubali hoja ya Mkapa, Mbunge Chadema asema hakuna kama Rais Magufuli
Akutwa na Sindano tumboni