Klabu za Chelsea na Tottenham zimepigwa faini kwa pamoja na chama cha soka nchini England FA, baada ya kukubali makosa matatu ya kushindwa kuwazuia wachezaji pamoja na maofisa wake wakati na baada ya mchezo ligi kuu ya soka nchini humo uliochezwa siku ya jumatatu.

Kiungo wa Spurs, Mousa Dembele amekumbana na adhabu pia ya kusababisha vurugu katika mchezo huo uliomalizika kwa matokeo ya sare ya kufungana mabao mawili kwa mawili.

FA imesema kuwa kitendo cha Dembele kumuingizia vidole machoni mchezaji wa Chelsea Diego Costa ni utovu mkubwa wa nidhamu.

The Belgian midfielder (left) appeared to gouge the Span striker's left eye in a touchline exchange Kiungo wa Spurs, Mousa Dembele akimfinya sehemu za jicho mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa.

Hiyo ina maana ”akikutwa na hatia” kufungiwa michezo mitatu pekee haitoshi.

Dembele, mwenye umri wa miaka 28, amepewa saa kadhaa za hii leo kujibu mashataka hayo huku kwa pamoja Chelsea na Tottenham wakipewa mpaka siku ya jumatatu ya juma lijalo.

Mwamuzi wa mchezo huo Mark Clattenburg hakuweza kutoa adhabu kwa Dembele kwa vitendo vyake lakini kamera za uwanjani zilimnasa mbelgiji huyo akiingiza vidole vyake kwenye macho ya Costa.

Katika mchezo huo zilitolewa kadi za njano 12 kutokana na vurugu zilizosababishwa na pande zote mbili.

Mauricio Pochettino could also be in trouble after entering the field of play on Monday nightMeneja wa Tottenham Mauricio Pochettino akiwaachanisha beki wake Danny Rose na kiungo wa Chelsea Willian

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino aliingia uwanjani kwa hatua kadhaa kwa lengo la kuwaachanisha beki wake Danny Rose na kiungo wa Chelsea Willian, huku pia Rose akihusishwa katika tukio lililosababisha mejeja wa Chelsea kuangushwa chini.

Spurs walihitaji kuifunga Chelsea ili kuweza kurudisha matumaini ya kutwaa taji la ligi kuu England lakini wakaishia suluhu hatua ambayo iliwawezesha Leicester city kujitangazia ubingwa.

Snura hana majanga na chura wake, awapa neno mashabiki
Wabunge wapigana ngumi bungeni