Mwenyekiti wa Chaumma, Hashim Rungwe Spunda ameungana na Chadema kumnadi mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni, Salumu Mwalimu na kuwaomba wananchi wampigie kula akidai kuwa mgombea wa CCM ni msaliti na hawapaswi kumchagua.

Rungwe ameilaumu Serikali ya awamu hii kufanya kazi zao kwa kuwatumia polisi kukamata watu na kuwaweka ndani.

”Tumeona tawala nyingi lakini mmeshawahi kuona utawala wa namna hii? Yaani polisi ndiyo wanafanya serikali ifanye kazi yaani bila ya polisi hawafanyi kazi, polisi ndiyo wamewekwa mbele yaani ukisema hivi unakamatwa” Amesema Rungwe.

Rungwe aliendelea kuelezea juu ya sakata lake la kukamatwa na polisi siku za karibuni.

“Mnakumbuka mimi nilikamatwa juzi juzi hapa yaani hakuna kitu chochote cha maana mpaka sasa mimi ni Wakili na Wakili kazi yake ni kusaini nyaraka, nimesaini nyaraka za watu na hao watu wenye pesa walikuwa wakitoa maagizo mlipe huyu na huyu na mimi nalipa sasa mimi nimefanya kosa gani? Hawa watu ni wabaya na haya ni mambo ya serikali ya CCM, hakikisheni kwamba serikali ya CCM mnaiondoa msikubali Mtulia awe Mbunge wenu. CCM ndiye wanaiharibu nchi hii” alisisitiza Rungwe.

Aidha ameongezea kuwa, “Serikali hii ya CCM inajidai sanaa inafanya propaganda kwenye Radio na kila mahali lakini mimi naomba niulize wangapi wamekuja hapa hawana kitu mfukoni, mna hela nyie? Wananchi hali zao mbaya watu hawana kitu.

Hivyo amewaomba wananchi kumchagua kiongozi kutokana na mambo anayoyafanya na kuwasisitizia wasimchague mgombea huyo toka chama cha CCM.

Video: Dkt. Slaa afunguka mazito baada ya kuapishwa
Diamond amjibu Zari, 'hujaacha tobo uliloniachia ni bonge la tundu'