Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inamshikilia aliyekuwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Sinamila iliyoko wilayani Bukombe mkoani Geita, Mashaka Lusotola kwa tuhuma za kupokea rushwa ya kuku kutoka kwa wazazi wa wanafunzi.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Amani Mwenegoha kumvua cheo cha ualimu mkuu mtumishi huyo akieleza kuwa amebaini walimu wa shule hiyo wamekuwa na tabia ya kuwaagiza wazazi kuku pindi wanapoandikisha watoto wao darasa la kwanza.

Alisema kuwa Mwalimu huyo alishindwa kuwadhibiti walimu walioko chini yake wasiendeleze vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na sheria.

Hata hivyo, mwalimu huyo alieleza kuwa amefurahishwa na hatua hiyo ya kuvuliwa ualimu mkuu huku akikifananisha kitendo hicho na ‘kumpiga teke chura’.

 

Mwanasheria azungumzia uzushi wa kifo cha Gwajima
Angalia video mpya ya wimbo wa Beyonce 'Formation'