Mbunge wa Suna Mashariki nchni Kenya, Junet Mohammed ametoa sauti ambayo ilimnasa Naibu Rais William Ruto akikiri kwamba nusura ampige Rais Uhuru Kenyatta kofi kuhusu uamuzi wa Mahakama wa Upeo kubatilisha uchaguzi wa urais wa 2017.

Mbunge huyo hakueleza chanzo cha sauti hiyo ambayo ilirekodiwa wakati wa mkutano wa faragha katika makazi ya DP Ruto huko Karen uliofanyika Ijumaa, Julai 1.

Yaliyomo kwenye rekodi hiyo yaliripotiwa kwa mara ya kwanza na gazeti la Daily Nation japo sauti hiyo haikuwekwa wazi.

Hata hivyo, Junet alicheza kanda hiyo kamili wakati wa mkutano wa mgombea urais wa Azimio Raila Odinga huko Ndhiwa, Homa Bay ambapo waliohudhuria walikuwa wametakiwa kuacha simu zao nje ya chumba.

Katika kanda hiyo, Ruto anasikika akicheka alipokuwa akizungumza kuhusu yale Rais alikuwa akifanya siku hiyo.

“Nilitoka hapa nikaenda Ikulu, sitaki kusema nilipofika huko alikuwa anafanya nini maana sisi ni wazee (anacheka) akaanza kunung’unika akisema hataki tena anataka kwenda kwa Ichaweri na kwamba tumuache awe.”

“Nilimtazama na kumwambia kuwa wewe! Nivile nilikuwa tu namheshumu bure ningempiga kofi kisha tukaacha tukaondoka?” DP alisema.

Junet alidai kuwa rekodi hiyo ilithibitisha kuwa nchi hii haitakuwa salama chini ya uongozi wa mtu ambaye angekuwa na ujasiri wa kumpiga kofi rais aliye madarakani.

Askari uhifadhi watakiwa kujenga uhusiano mzuri na wananchi
TBS, wananchi na wafanyabiashara 'uso kwa uso' sabasaba