Klabu ya Ruvu Shooting ipo kwenye mchakato wa usajili ila imeweka wazi kuwa wachezaji kutoka timu za Simba na Yanga wasahau kuichezea timu hiyo kwani hawana uvumilivu na hawajitumi.

Ruvu Shooting imepanda kushiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao na bado inaendelea kufundishwa na Tom Olaba ambaye ni Kocha Mkuu.

Msemaji wa Klabu hiyo, Masau Bwire, alisema hawawezi kusajili wachezaji kutoka timu hizo kongwe kwani licha ya kutocheza kwa kujituma pia nidhamu zao ni mbovu.

“Hatuna mpango wa kusajili makapi ya Simba na Yanga kwani wachezaji hao huwa mara nyingi hawana moyo wa kupambana na pia nidhamu zao ni mbovu,” alisema Masau.

Alisema kocha wao mkuu, Olaba amependekeza kikosi chao kusajili wachezaji saba wenye vipaji ambapo uongozi unalifanyia kazi jambo hilo ili kutimiza matakwa yao ya kuwa na timu imara msimu ujao.

Dk. Migiro ateuliwa Balozi Uingereza
Hans Pope Amshangaa Jerry Muro Kulivimbia Suala La Rushwa

Comments

comments