Shirika la Foundation for Civil Society (FCS), limetoa ruzuku ya Shilingi shillingi 3,957,301,580 sawa na Bilioni nne (4) kwa asasi za kiraia (AZAKI), 89 Tanzania bara na visiwani kutekeleza miradi ya kimaendeleo.

Utekelezaji wa miradi hiyo, utakuwa chini ya programu za utawala bora katika sekta za maji, elimu, afya na kilimo, usawa wa kijinsia, ujumuishwaji wa vijana na watu wenye ulemavu, na ujenzi wa amani na mshikamamo wa kijamii kwa mwaka 2022-2023.

Akizungumza katika warsha, kwa AZAKI hizo zilizochaguliwa kupata ruzuku jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Francis Kiwanga amesema wamejitika katika kuhakikisha miradi inayofadhiliwa inawasaidia wananchi katika kuboresha maisha yao na kukuza sekta ya asasi za kiraia.

Takwimu sensa kusaidia tathmini za Wafanyabiashara

‘’FCS imepitisha mpango mkakati mpya wa mwaka 2022-2026 ambao unataka kuona wananchi waliowezeshwa, wastahimilivu, wanaowajibika na wanaopata haki za kiuchumi, kijamii na kuboresha ubora wa maisha yao,” amesema Kiwanga.

Ameongeza kuwa, “Tutaweza kufanikisha malengo yetu kwa kuchangia maendeleo endelevu na shirikishi nchini Tanzania kwa kuimarisha uwezo, kugawana rasilimali, na ushirikiano wa kimkakati na AZAKIi, vikundi vya jamii pamoja na watendaji wengine wa maendeleo.’’

Meneja Programu Utawala Bora FCS, Edna Chilimo amezungumzia ruzuku mbalimbali kwa kusema FCS imetoa ruzuku kwa AZAKI ikiwemo zilizo ndogo, za kati na za kimkakati na kwamba wamekuwa wakifanya kazi na mashirikia madogo na viongozi wa klasta za programu ambao wanafanya kazi katika ngazi ya taifa, asasi za Kijiji, Kata na Wilaya.

Serikali yaidhinisha mgao wa Taulo za kike bure

Amesema, baadhi ya misingi ya ubia ni pamoja na uelewa wa pamoja, malengo ya pamoja, na kuaminiana ili tuweze kufikia malengo ya pamoja huku wakiwajengea uwezo Azaki ili ziweze kutekeleza miradi, kujiongoza, iwe imara, na inayotambulika.

Tunajengea uwezo Azaki ili kuweza kuandaa na kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali, Sekta binafsi, Mwananchi na Azaki nyingine.

“Tumekuwa Walezi wa sekta ya AZAKI. Tumechangia ukuaji wa sekta, miaka ya nyuma tulitoa fedha kwa Azaki kujisajili na sasa kuna Azaki zimekua, kutoka shirika dogo hadi kuwa mashirika makubwa yenye sifa,” amefafanua Chilimo.

Tangu kuanzishwa kwake miaka 20 iliyopita, FCS imechangia kwa kiwango kikubwa katika kuimarisha uwezo wa sekta ya kiraia nchini Tanzania na kuwezesha asasi za kiraia kupata chachu ya maendeleo na wananchi kuwa mstari wa mbele katika kuimarisha utawala wa kidemokrasia nchini.

Kenya: Wagombea walivyowasili Bomas tayari kwa matokeo

Kenya: William Ruto Rais mteule, amshukuru Mungu
Matokeo Kenya: Hali ya utulivu yarejea matokeo yaanza kutolewa