Mamlaka ya Mapato ya Rwanda imetangaza kupiga mnada mali za kampuni inayomilikiwa na familia ya Diane Rwigara, mwanamke aliyetaka kugombea urais mwaka jana.

Mamlaka hiyo imeeleza kuwa itapiga mnada mali hizo za kampuni ya sigara ya Premier Tobacco Company, Machi 28 mwaka huu, ili kufidia deni la kodi ya dola za kimarekani milioni sita ($6 million).

Deni hilo linadaiwa kuwa ni mlindikano wa ukwepaji kodi wa kampuni hiyo kwa miaka kadhaa.

Familia ya Diane anayeshikiliwa na vyombo vya usalama kwa tuhuma mbalimbali imedai kuwa ilianza kufuatiliwa baada ya mwanamke huyo kutangaza nia ya kugombea urais Agosti 4 mwaka jana.

Hata hivyo, Diane hakufanikiwa baada ya kushindwa kufikisha vigezo vilivyowekwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Siku kadhaa baadaye, alitiwa mbaroni pamoja na mama yake kwa makosa ya uchochezi pamoja na kugushi.

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Machi 19, 2018
Manara: Hatutakuwa wazalendo kwa Yanga