Serikali ya Rwanda imesema kuwa imepiga hatua katika kuboresha haki za binadamu kwa kutekeleza makubaliano ya kimataifa ya Geneva kuhusu haki za binadamu.

Nchi hiyo imetangaza hatua hiyo wakati kukiwepo ukosoaji mkubwa wa kimataifa kuhusu ukosefu wa uhuru wa kutoa maoni nchini humo.

Waziri wa sheria na mwanasheria mkuu wa Rwanda, Johnston Busingye amesema kuwa katika mikataba 50 ya Geneva kuhusu kuheshimu haki za bidamu nchi ya Rwanda imekwisha tekeleza mikataba minane kati yake kwa kiwango cha asilimia 100 huku ile iliyosalia ikiendelea kutekelezwa kwa kiwango cha kati ya asilimia 80 hadi 90.

“Tunafurahi kwa sababu tunaendelea kutekeleza kwa kiasi kikubwa makubaliano ya kimataifa kuhusu haki za binadamu kama ilivyosainiwa kule Geneva na tutaendelea kufanya hivyo hadi mikataba yote 50 tuliyosaini tuitekeleze kikamilifu,”amesema Busingye

Aidha, waziri huyo ameyasema hayo wakati kukiwepo na malalamiko ya mashirika ya kutetea haki za binadamu kuhusu ukosoaji wa haki za binadamu na ukosefu wa uhuru wa kutoa maoni nchini Rwanda.

Hata hvyo, Mwanasheria anayetetea haki za binadamu nchini humo, Andrew Kananga amesema kuwa kutokana na hali ilivyo nchini Rwanda hakuna tishio lolote la hatari kwa haki za binadamu kutokana na mabadiliko ya sheria ambayo yamekuwa yakibinywa kila kukicha.

LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Februari 8, 2018 | Maswali kwa Waziri Mkuu
Polisi Congo-DRC watuhumiwa kufanya mauaji mgodini