Siku chache zikiwa zimepita baada Mahakama ya ICC kuzishtaki nchi za Uganda na Djibouti kwa kushindwa kumkamata Rais wa Sudan Omar al Bashir alipozuru katika nchi hizo.

Waziri wa maswala ya nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo amesema kuwa ombi la Mahakama ya uhalifu wa kivita ICC kupitia kwa barua rasmi walioiandika siku mbili zilizopita haina uzito wowote.

Serikali ya Rwanda imetupilia  mbali ombi la mahakama hiyo yenye makao yake makuu huko Hague Uholanzi ICC ya kumkamata rais wa Sudan Omar al-Bashir.

bashar

ICC inamtaka bwana Bashir akamatwe kwa makosa ya mauji ya halaiki katika jimbo la Darfur Sudan, japokuwa amekanusha madai yote dhidi yake.

Rais Bashir atahudhuria kongamano la viongozi wa Afrika linaloandaliwa mjini Kigali mwisho wa wiki hii.

Afande Sele amzungumzia Mrithi wa 'Ufalme wa Rhymes', awabeza marapa
Zoezi la Ukamataji Omba Omba Jijini Dar Laendelea