Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Richard Sezibera amekanusha taarifa zilizozagaa kwamba nchi hiyo imefunga mpaka wake na Uganda.

Ameyasema hayo Jijini Kigali nchini humo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya wizara ya mambo ya nje,

”Shughuli ya ujenzi wa barabara katika mji wa mpakani wa Gatuna umefanya magari kuelekezwa katika mpaka wa Kagitumba, ingawa uhusiano wetu bado mzuri, lakini hatujafunga mpaka,”amesema Sezibera

Aidha, amesema kuwa Rwanda inaendelea na majadiliano na majirani zake kuhusiana na masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na kuzuiliwa kwa raia wake nchini Uganda.

Pia amekanusha taarifa ya vyombo vya habari inayodai kuwa taifa hilo limepeleka vikosi maalum vya kijeshi katika mpaka wake na Uganda tangu ilipochukua hatua ya kuifunga.

Hata hivyo, Alhamisi iliyopita mamlaka ya mapato ya Rwanda iliamrisha maroli ya mizigo kutotumia tena mpaka wa Gatuna kwa madai ya shughuli za ujenzi wa kituo kimoja cha mpakani ‘one stop border’ baina yake na Uganda.

Wasusia majeneza yenye miili ya marehemu mpakani
Zidane atajwa kuwa ‘shujaa’ wa kuinoa Chelsea