Raia katika jiji la Kigali, Rwanda leo wameanza kutekeleza amri ya kutotoka nje kwa siku 15 kufuatia kushuhudiwa kwa ongezeko la maambukizi ya Covid 19 nchini humo na idadi kubwa ya vifo ndani ya siku 50.

Biashara, Ibada na mikusanyiko imepigwa marufuku huku wafanyakazi wa Serikali na sekta binafsi wakifanyia kazi nyumbani.

Hadi sasa Rwanda imefikisha vifo 142 vilivyosababishwa na Corona huku wagonjwa wapya elfu 4 wakiwa wamegundulika ndani ya hizo siku 50 na kufikisha idadi ya visa elfu 11 tangu kugundulika kwa mgonjwa wa kwanza wa Corona nchini humo.

Watu wanaruhusiwa kutoka kununua chakula au matibabu na zaidi ya hapo ni kwa wale tu watakaokuwa na kibali kinachotolewa na Polisi.

Shule zote Kigali na Vyuo Vikuu vya Serikali na binafsi vimefungwa, baadhi ya hoteli zitaruhusiwa kupokea wageni kutoka nje ya nchi ambao hata hivyo na wao watafuata masharti haya ikiwemo amri ya kutotoka nje usiku inayoanza saa kumi na mbili jioni.

AC Milan yamnasa Mario Mandzukic
Azam FC yafanya mabadiliko