Serikali ya Rwanda imetangaza marufuku ya kutoka nje ya muda wa siku 10 katika mji mkuu wa Kigali na wilaya nane baada ya ripoti za vifo na wagonjwa wa corona kuongezeka.

Maofisa wa afya wamesema kusambaa kwa wimbi la tatu la kirusi kipya cha Delta ndio kinafanya taifa hilo kuwa na hali mbaya zaidi.

Watu wametakiwa kutotoka nje ya nyumba zao kuanzia Jumamosi tarehe 17 mpaka tarehe 26 Julai, ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Hatahivyo biashara, shughuli za umma, usafiri, shule, michezo na burudani vyote vimefungwa na mazishi yanatakiwa kuhudhuriwa na watu 15 tu.

Wiki nne zilizopita, taifa hilo limerekodi watu elfu moja waliopata maambukizi ya corona kwa siku na siku saba zilizopita hali ilikuwa mbaya zaidi.

Paka hivi sasa Rwanda imerekodi visa zaidi ya 50,000 vya covid , na zaidi ya waathirika 600 na huku zaidi ya watu mia nne wamepata chanjo.

RC Makalla awataka wakurugenzi kuwawezesha maafisa ushirika kutimiza majukumu yao
Hatima ya Hausiboi aliyeua familia Dar