Rwanda imezundua gari lake la kwanza aina ya Volkswagen lililotengenezwa na kiwanda kilichopo nchini humo katika mji mkuu wa Kigali.

Gari hilo aina ya Polo ni la kwanza kutengenezwa katika kiwanda hicho huku kampuni hiyo ya magari ya Ujerumani ikitarajiwa kutengeza magari 5,000 katika awamu ya kwanza ambayo pia itatengeneza magari yake aina ya Passat, Tiguan, Amarok na Teramont

Aidha, Kampuni ya magari ya Volkswagen ambayo ndio kubwa zaidi barani Ulaya imefanya uwekezaji wa $20m (£15m) nchini Rwanda unaotarajiwa kuajiri watu 1000.

Hata hivyo, Kampuni hiyo inapanga kuuza magari hayo mbali na kuyatumia kama teksi ambapo wateja watawasilisha maombi ya kutaka huduma hiyo kupitia simu zao.

Magufuli, Obama kufanya ziara nchini Kenya
Moto wateketeza soko,15 wafariki dunia