Kiungo wa zamani wa Manchester United, Ryan Giggs amesema anaamini kama winga wa Inter Milan, Ivan Perisic atatua ndani ya United basi ataongeza ushindani mkali kwenye kikosi hicho.

Kumekuwa na taarifa kuwa winga huyo anawaniwa na United kwa nguvu huku ikielezwa kuwa anaweza kusajiliwa hapo kwa pauni milioni 44.

Giggs amesema, mchezaji huyo akitua United basi itakuwa ni changamoto kubwa kwa Marcus Rashford, Henrikh Mkhitaryan na Anthony Martial ambao watatakiwa kuboresha uwezo wao ili kumpa ushindani katika kikosi cha kwanza.

“Kama akija, watatakiwa kujipanga, kutakuwa na presha kubwa, atakayepewa nafasi kisha akashindwa kuitumia atapoteza nafasi mchezo unaofuata,” alisema Giggs.

Mambosasa: Hatuna mpango wa kumkamata Lissu
Vanessa afunguka mapenzi yake na Jux yalikuwa yakisela