Meneja msaidizi wa klabu ya Man Utd Ryan Giggs, huenda akaondoka Old Trafford endapo Jose Mourinho atatangazwa kuwa mbadala wa Louis Van Gaal, ambaye yu tayari kuachia ngazi klabuni hapo.

Giggs anajiandaa kufikia maamuzi hayo, kufuatia uvumi uliosambaa tangu mwishoni mwa juma lililopita, ambapo inadaiwa Mourinho huenda akatangazwa na uongozi wa Man Utd wakati wowote juma hili.

Giggs ambaye ameitumikia Man Utd kwa miaka miaka 29 kama mchezaji kabla ya kuwa sehemu ya benchi la ufundi, anadaiwa kutokua tayari kufanya kazi na Mourinho kwa kuamini hawatoendana na mreno huyo.

Taarifa za Giggs, kuondoka endapo Mourinho atakabidhiwa kikosi, zilianza kusikia kitambo, hasa fununu za kuondoka kwa Louis Van Gaal zilipoanza kuchukua nafasi mwanzoni mwa mwaka huu.

Hata hivyo taarifa nyingine zinadai kwamba Giggs alitaka kuona uongozi wa Man Utd ukimkabidhi jukumu la kuwa meneja wa klabu hiyo, baada ya kuondoka kwa Van Gaal kwa kuamini tayari alikua ameshaiva kuwa mkuu wa benchi la ufundi la klabu hiyo ambayo alianza kuitumikia akiwa na umri mdogo.

Giggs alianza kuwa sehemu ya benchi la ufundi la Man Utd, tangu utawala wa David Moyes ambaye alikabidhiwa jukumu la umeneja baada ya kuondoka kwa Sir Alex Ferguson.

David Moyes Kurejea Katika Soka La England?
Euro 2016: Roman Neustadter Atajwa Kikosini