Jumla ya watu saba wamefariki na wengine 21 kulazwa katika hospitali ya mkoa mjini Dodoma baada ya kuzuka ugonjwa ambao hadi sasa madaktari hawajatambua  tiba yake.

Kufuatia kuibuka kwa ugonjwa huo tayari kumetengwa wodi maalum katika hosptali ya taifa ya rufaa ya Dodoma katikati mwa Tanzania ambapo pia karantini imewekwa na hakuna anayeruhusiwa kukaribia mahali hapo zaidi ya madaktari ambao nao pia wanaingia kwenye wodi kuwaona wagonjwa kwa tahadhari kubwa.

tanzania

Hofu na wasi wasi umezidi kutanda huko mkoani Dodoma katikati mwa Tanzania baada ya kuibuka kwa ugonjwa usiojulikani huku dalili za ugonjwa huo ukiwa ni pamoja na kutapika, kuharisha, ngozi na macho kuwa ya njano pamoja na kuumwa na tumbo.

Hata hivyo katika taarifa iliyotolewa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Ummy Mwalimu amesema tayari Daktari bingwa kutoka hospitali ya taifa muhimbili ameshakwenda Dodoma kwa ajili ya kuongeza nguvu pamoja na wataalamu wengine kutoka ofisi ya Mkemia mkuu wa serikali.

ummy-

Ameendelea  kutoa rai kwa jamii, kuacha kutiliana wasiwasi na kushutumiana kwa kupigana badala yake wahimizane kwa yeyote yule atakayeumwa na dalili kama zilizotajwa hapo juu awasili au kumpeleka kituo cha Afya ili aweze kusaidiwa kwa haraka.

Aidha kutokana na ufuatiliaji na uchunguzi unaoendelea kufanyika, ugonjwa huu unaweza kuhusishwa na ulaji wa vyakula vyenye sumu kuvu (Aflatoxins), kutokana na matumizi ya vyakula vya namna mbalimbali visivyohifadhiwa vizuri. Hii ni kinyume na mtazamo wa wale wanaosema kuwa ugojwa huu ni kimeta. Amesema Mh. Mwalimu.

Unyama: ISIS wamchinja msichana wa miaka minne kwa 'utani' aliofanya mama yake
Hans Poppe: Yanga Wanajifanya Wanajua Kila Kitu