Watu saba wameuawa kwa risasi, wakiwemo watoto wakati wa sala ya Ijumaa (Januari 27, 2023), kwenye sinagogi moja lililopo Mashariki mwa Jerusalem, ikiwa ni muendelezo wa machafuko ambayo yameibua mzozo kati ya Israel na Palestina.

Taarifa ya Polisi nchini Palestina imeeleza kuwa, tukio hilo, lilitekelezwa na mtu mmoja ambaye aliingia katika sinagogi hilo la Neve Yaakov na kisha kuwafyatulia risasi waumini waliokuwa wakishika sabato ya Kiyahudi.

Mtuhumiwa aliuawa na Polisi wakati akijaribu kutoroka huku akifyatua hovyo risasi ambazo ziliwajeruhi watu. Picha ya Ahmad Gharabli/AFP.

Katika tukio hilo, watu wengine watatu walijeruhiwa wakiwemo wawili ambao wako katika hali mbaya na mtuhumiwa huyo (21), aliuawa na Polisi wakati akijaribu kutoroka huku akifyatua hovyo risasi ambazo zilipelekea kuwajeruhi watu hao.

Tukio hilo, linakuja ikiwa ni siku moja baada ya wanajeshi wa Israel kuwaua Wapalestina tisa, wakati wa uvamizi wa kijeshi huko Jenin, ilipofanyika operesheni mbaya zaidi kuwahi kutokea katika Ukingo wa Magharibi ndani ya miongo miwili.

Wataalamu Mawasiliano watakiwa kulitumikia Taifa kwa weledi
Serikali kusafirisha Duma 100 nje ya nchi