Jumla ya Wanachama Saba wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini wamechukua na kurudisha fomu za kuwania nafasi ya udiwani wa kata ya Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga.

Akitoa taarifa hiyo Katibu Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Said Bwanga amewataja waliochukua na kurudisha fomu hizo kuwa ni pamoja na Pendo Sawa, Samwel Jackson, Gelewa Njelo,, Solomon Najulwa, Dotto Joshua, Victa Thobias na Hamis Hamis.

Hata hivyo Bwanga amefafanua kuwa idadi ya waliochukua fomu ilikuwa wanachama nane (8) lakini Mmoja kati yao hakurudisha fomu hiyo ambaye ni Dkt. Ezekiel Meshaki.

Katibu mwenezi huyo ameeleza mchakato wa kumpata Diwani wa kata ya Ndembezi utaanza rasmi kesho ukitanguliwa na zoezi la kura za maoni ili kumpata mgombea mwenye sifa.

“Tunaanza rasmi kesho tutaendelea na mtiririko kesho tunaanza na ngazi ya kata,Wilaya baadae Mkoa ndipo moja kwa moja tutaweza kupendekeza jina ambalo litaingia katika kinyang’anyiro kupitia Chama Cha Mapinduzi,” Amesema Katibu Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Said.

Aidha Bwanga amesema wote waliochukua fomu hizo ni wananchama halisi ,wanachama hai na wanasifa zote za kugombea nafasi ya uongozi.

Mchakato huo unafuatia aliyekuwa diwani wa kata hiyo David Nkulila kufariki Dunia Mwezi uliopita ambaye pia alikuwa ni Meya wa Manispaa ya Shinyanga.

Sudan:Mafuriko yaua watu zaidi ya 70
Young Africans matumaini kibao