Aliyekuwa mbunge wa Ubungo, Sued Kubenea, kupitia tiketi ya CHADEMA ambaye amehamia ACT- WAZALENDO ametaja sababu iliyomfanya asigombee jimbo hilo kwa mwaka huu ni kutokana na migogoro iliyokuwepo katika chama hicho.

Ambapo amesema kuwa hakuwa tayari kushiriki kwenye dhambi ambayo ingesaidia jimbo hilo kwenda Chama cha Mapinduzi (CCM) .

“Miongoni mwa sababu iliyopelekea kutokugombea jimbo hilo tena ni kutokana na migogoro iliyokuwepo kwenye chama changu,” alisema Kubenea.

Aidha ameeleza kuwa licha ya kwamba hakuchukua fomu ya kuwania Ubunge kupitia CHADEMA, lakini hiyo haimzuii yeye, kugombea jimbo hilo kupitia chama kingine kwa kuwa michakato ndani ya vyama vingine haijafungwa.

Ikumbukwe Julai 18, 2020 Kubenea aliondoka Chadema na kujiunga na Chama cha ACT-Wazalendo.

DC atoa neno kuhusu Uchaguzi Mkuu
Mazingiza akabidhi ofisi Simba SC