Kuna baadhi ya watu wamekata tamaa katika utunzaji wa nywele zao kwa kile wanachoamini kuwa nywele zao zimegoma kukua , wengine hukimbilia kuweka dawa.

Hivyo kwa wale wenye nywele za asili yaani zisizo na dawa zifuatazo ndio sababu zinazosababisha nywele kutokukua.

kwa watu wenye nywele asilia kuna muda utaona nywele zako hazishtuki wala kurefuka , la hasha wala usikate tamaa aina hii ya nywele huwa na tabia ya kunywea na kurudi chini hivyo sio kwamba ni fupi lakini zinakuwa zimerundikana kwa ndani.

Tabia mbovu ya utunzaji wa nywele.

Unaweza kuhisi kama unatunza nywele zako vizuri kumbe ndio kwanza unaziharibu kabisa, wengi wamezoea kutumia moto katika kuzi-style nywele zao, kuweka rangi kwenye nywele au kusuka na kuweka style zinazovua sana nywele na kufanya nywele zikatike.

Nywele kuwa kavu sana na kukosa unyevunyevu

ni lazima kujua aina ya nywele zako ili kujua jinsi ya kuzihudumia, kwa kawaida nywele kavu huwa zina katika muda mwingine huweza kukatika kwa speed ileile inayokuwa nayo kwaio kile kinachoingia ndio kinachotoka .hapo tunakuwa unalalamika tu kuwa nywele zako zimedumaa.

Zingatia muda wa kukata ncha.

Kuna muda nywele zitataka kupunguzwa ncha ili ziendelee kukua, inakuwa kama mti unaotaka kupunguzwa matawi.Ukataji wa ncha utoa nywele za mbele ambazo mara nyingi zinakuwa zimeharibika na usababisha zile za nyuma zisikuwe kwa wepesi.

Jua mzunguko wako wa nywele kukua

Sio kila nywele hukua haraka kama vile unavyofikiri, Kuna watu wanamzunguko mrefu na wengine wanamzunguko mkubwa wa nywele kukua, hii ni kulingana na genetics ya mtu.

Baadhi ya wataalamu wanasema kuwa kuna mzunguko wa ukuaji wa nywele wa miaka 2 hadi 6 na nywele uanza mzunguko tena.

Uchaguzi mbaya wa vifaa vya kutunzia nywele

Jaribu kutumia vifaa bora katika kutunza nywele zako, usilazimishe kutumia kitana wakati nywele zako na kuchana na chanuo.Na hata kama ni chanuo basi tumia lenye meno mapana.Vile vile jaribu kutumia mafuta mazuri yanayoendana na nywele zako.Ukiona unashindwa kutambua basi jaribu kuonana na

 

Ashley Cole ampa muda Unai Emery
Video: Ridhiwani achangia milioni 5 ujenzi wa ofisi za CCM Kata ya Kiwangwa