Mshenga wa ndoa ya Nuh Mziwanda na Nawal anayefahamika kama HK, amefunguka na kutaja sababu kubwa iliyopelekea ndoa hiyo kuvunjika.

HK ametaja sababu kubwa kuvunjika ndoa hiyo ni kumekuwa na mvutano wa kidini baina ya Nawal na familia ya Nuh Mziwanda hasa mama mzazi wa Nuh aliyedai haitambui ndoa hiyo, na inasemakana kuwa hakuhudhuria ndoa ya mwanae Nuh kwa madai ya kuwa hakupata taarifa ya ndoa hiyo.

”Ukiacha tofauti zao zilizokuwa zikitokea, kilichotokea sasa hivi wamekuwa wanavutana sana Nuh alikuwa anataka Nawal akakae kwa mama yake na Nawal hataki kukaa kwa mama yake Nuh kwa sababu mama yake Nuh anasema haitambui ndoa yao kwa sababu mwanae ni mkristo na hajui kwa nini kabadilisha dini”. Ameseam HK.

”Hiyo ndio kesi kubwa nilikuwa nikivutana nayo sana mpaka dakika ya mwisho niliongea na mama yake Nuh kwenye simu akanambia mwanangu umefanya makosa sana kumuozesha mwanangu bila mimi mwenyewe kujua.

Aidha HK alitoa ushauri kwa Nuh na aliyekuwa mke wake Nawal na kuwaomba wasiachane kwa shari kwani tayari wanakiumbe kinachowaunganisha pamoja (Anyagire) hivyo kama wazazi ambao walioana kwa heri basi na kuachana waachane kwa heri ili wasimpe mtoto wao mazingira magumu pale atapokuwa mkubwa.

 

 

 

Ndoa ya Irene Uwoya nayo mbioni kusambaratika
JPM awataka wapinzani mkoani Tanga kutojisifia