Jeshi la Magereza nchini limetoa taarifa za sababu ya kuachiwa kwa Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chadema, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu kabla ya miezi yake mitano aliyohukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi kukamilika.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa sababu za Mbunge huyo amechiwa  huru kwa msamaha uliotolewa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli April 26 mwaka huu katika maadhimisha ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Baadhi ya wafungwa akiwemo Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi waliotumikia kifungo chao angalau robo ya hukumu yao walipatiwa msamaha wa 1/3  ya kifungo chao.

Soma taarifa iliyotolewa hapo chini kwa vyombo vya habari.

 

Kuteuliwa sio tatizo, ukishindwa tunakurudisha- JPM
Wema Sepetu amcharukia Hamissa Mobeto

Comments

comments