Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeeleza kuwa Kampuni ya ndege ya Fastjet ilikosa leseni mpya kwa sababu ilishindwa kuwasilisha maombi yao ndani ya muda uliokuwa umepangwa, ambao ni Aprili, 2019.

Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari ameeleza kuwa walipokea maombi ya Fastjet siku moja kabla ya Mei 18, 2019, siku ambayo Bodi ya Wakurugenzi ilikutana kujadili maombi yaliyokuwa yamewasilishwa ndani ya muda.

“Katika hali ile, ilikuwa ngumu kwetu kuyafanyia kazi maombi yao na kuyawasilisha katika kile kikao, kwahiyo maombi hayo ilibidi yasogezwe hadi Novemba ambapo kutakuwa na kikao kingine cha Bodi,” The Citizen wamemkariri Johari.

Kwa mujibu wa tangazo ambalo TCAA ililitoa hivi karibuni, Fastjet walikuwa wamewasilisha maombi yao yakiwa na ratiba ya safari walizopanga kufanya ndani na nje ya nchi. Baadhi ya ya safari ya za nje ya nchi zilizotajwa na kampuni hiyo ni kwenda Johannesburg, Lubumbashi, Lusaka, Kigali, Moroni na Dubai.

Leseni ya Fastjet ilikuwa imekwisha tangu Januari 3, 2019, na shirika hilo limesitisha safari zake tangu mwaka jana kutokana na matatizo ya kifedha na mambo mengine.

Fahamu sababu ya maumivu kwenye korodani kuwa chanzo cha ugumba
DataVision International yashinda tuzo ya ‘Brand Leadership’ Afrika Mashariki

Comments

comments