Wasanii wa muziki nchini hivi karibuni walipinga uamuzi wa serikali wa kuvitaka vituo vyote vya redio na televisheni kuwalipa mirabaha kwa kucheza nyimbo zao redioni.

Uamuzi huo uliwashangaza wengi kwani kutopata sitahiki kwa kazi zao kilikuwa kilio cha wasanii hao cha muda mrefu kabla ya kuhakikishiwa na waziri wa habari, utamaduni, michezo na wasanii, Nape Nnauye aliyevitaka vituo vyote kuanza kuwalipa wasanii kuanzia Januari Mosi mwaka huu.

Rapa wa kundi la Weusi, Nikki wa Pili alieleza sababu zilizopelekea wasanii hao kukataa mpango huo, alipokuwa anaongea na Planet Bongo ya East Afrika Radio.

Hizi ndizo sababu zilizotajwa kama zilivyowekwa kwenye akaunti ya Instagram ya GraysonGideon:

Kwanza kampuni ya CMEA iliyopewa tenda hiyo inamilikiwa na kampuni ya #PUSHMOBILE ambayo wasanii wameshuhudia kua ina historia mbaya ya kuwaibia wasanii kwahyo hawawez kuwaamini tena.

Pili Sheria iliyounda COSOTA inasema lazima iundwe na kusimamiwa na wasanii wenyewe lkn haipo hivyo.kwahyo wasanii wanataka sheria ichukue mkondo wake na cosota isimamiwe na iongozwe na wasanii.

Pia bodi ya COSOTA haiundwi na wasanii na pia utendaji wa COSOTA siyo wa kurizisha ikiwemo kuwashauri wasanii issue za kimuziki ni jukumu lao lkn hawafanyi hivyo. -Kingine ni mazingira ya ulipaji mirabaha yanaonekana hayapo tayari.mfano wanasema Muziki utakaopigwa uwe wa nje au ndani (_ya nchi)utalipiwa,wakati huo huo wanasema ili wimbo ulipiwe lazima usajiliwe COSOTA na #CMEA ,lakini ukwel in kua nyimbo nyingi za nje na za nyumban hazijasajiliwa Popote kati ya taasisi hizo. -Kadhalika wanasema maudhui ya #Media za nyumbani 60% nyumbani na 40% ya nje na sheria hii imekuwepo kwa miaka mingi lakini ukiangalia uhalisia hasa kwa vituo vya #TV hapa Bongo maudhui yake 80% ni ya nje.

Kwamaana hiyo usimamizi huo haupo na wasanii hawawezi kusaini na kukubalina na mambo yasiyokuwepo kiuhalisia. -mwisho Ukiangalia hii sheria wanasema ni makubaliano ya kiukanda wa #AfricaMashariki kuwa media zipige 60% local content lakini ukiangalia #kenya mambo ya mirabaha yalipoanza media zilianza kupiga 80% maudhui ya nje na kwahyo hii sheria haina #Uhalisia.

Saudi Arabia Yashambulia ubalozi wa Iran
Mashabiki wa Ali Kiba waivimbia MTV Base