Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita, leo Novemba 16, 2021 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha katika kesi ya Uhujumu Uhumi inayomkabili mara baada ya kushindwa kufika katika Mahakama hapo mara tatu mfululizo

Sabaya na wenzake wamefikishwa mahakamani hapo saa 9:38 asubuhi, ambapo awali kuanzia Novemba 3 hadi 5, 2021 alishindwa kufika ikidaiwa kuwa anaumwa.

Wakili Mosses Mahuna, amewaeleza waandishi wa habari nje ya mahakama kuwa mtuhumiwa huyo anasumbuliwa na vidonda vya tumbo pamoja na uti wa mgongo ambapo alidai kuwa alipata ajali akiwa kazini.

Jana Jumatatu kesi hiyo ilishindwa kuendelea kusikilizwa baada ya watuhumiwa hao kutokufikishwa mahakamani hapo.

Hakimu Mkazi Patricia Kisinda anayesikiliza kesi hiyo namba 27, 2021 aliiahirisha hadi leo ambapo shahidi wa tisa wa Jamhuri ataanza kutoa ushahidi wake.

Katika kesi hiyo watuhumiwa wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Mabomu tena Kampala
Kumwembe: Mashabiki wa soka kuweni na heshima