Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha imewakuta na kesi ya kujibu aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya pamoja na wenzake 6 kwenye kesi ya uhujumu uchumi ambapo Hakimu Dkt Patricia Kisinda amesema Mahakama imepitia vielelezo 12 pamoja na mashahidi 13 walioletwa na upande wa jamhuri katika kuthibitisha mashtaka yanayowakabili Washitakiwa ambapo imewakuta na kesi ya kujibu.

Akitoa uamuzi huo mdogo, Hakimu Kisinda amesema baada ya mahakama kupitia vielelezo hivyo na mashahidi vilivyotolewa kuthibitisha makosa yanayowakabili na baada ya kujiridhisha imeona washitakiwa wote wana kesi ya kujibu.

Hakimu Kisinda ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 17 mwaka huu ambapo watuhumIwa hao wataanza kujitetea.

Akiongea kwa niaba ya Washtakiwa wote, Wakili wa upande wa utetezi wakili Moses Mahuna amesema watakuwa na Mashahidi wasiopungua kumi na watajitetea chini ya kiapo.

Washitakiwa hao wanakabiliwa na makosa matano la ambapo wakidaiwa Januari 22, 2021 ni kuongoza genge la uhalifu na kosa la tano ambalo ni utakatishaji fedha linawakabili washitakiwa wote saba  wanadaiwa kupata Sh 90 milioni kutoka kwa mfanyabiashara Francis Mrosso, huku wakijua kupokea fedha hizo ni zao la kosa la vitendo vya rushwa.

Sabaya peke yake ameshtakiwa ka kosa la pili,la tatu, nne kwa kujihusisha na rushwa ambapo anadaiwa kuchukua Sh 90 milioni matumizi mabaya ya ofisi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro.

Serikali yapokea dawa kutoka Misri
Aliyesajiliwa Simba SC kutangazwa leo