Jumuiya ya Maendeleo ya Mataifa ya Kusini mwa Afrika-SADC imetoa wito wa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa na kuhesabiwa upya kwa kura kuhesabiwa tena katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC, rais Edgar Lungu wa Zambia amesema kuwa jumuiya hiyo inazingatia kwa makini wasiwasi uliojitokeza kuhusiana na matokeo ya awali yaliyotangazwa na kutilia mkazo kura zihesabiwe upya akisema hiyo ndio njia pekee ya kutuliza wasi wasi wa aliyeshinda na pia wa walioshindwa.

Aidha, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC inayozijumuisha pia nchi za Afrika Kusini na Angola miongoni mwa wanachama wake ina masilahi makubwa ya kiuchumi katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambayo pia ni mwanachama.

Wasi wasi wa jumuiya ya kimataifa unatokana na msimamo wa Kanisa Katoliki-Taasisi yenye ushawishi mkubwa kabisa nchini humo, ililoutaka Umoja wa Mataifa uchapishe ripoti zote za uchaguzi ili kuondoa wasiwasi uliopo kwasasa.

Kwa Mujibu wa Mkutano wa Baraza la Taifa la Maaskofu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-CENCO, matokeo yaliyotangazwa na tume huru ya uchaguzi CENI hayalingani na matokeo yaliyokusanywa na wasimamizi 40.000 wa taasisi hiyo.

 

Serikali yataifisha mashamba ya kampuni ya Mohamed Enterprises
Aweso amsukuma ndani mhandisi wa maji Muleba