Chama cha michezo kwa watu wenye ulemavu wa viungo Zanzibar (SADZ) wamekabiliwa na mashindano makubwa ya Kilimanjaro Marathon ambapo walipata mualiko kutoka huko kwa wenzao Tanzania bara,  mashindano ambayo yataanza tarehe 27 ya mwezi huu wa pili.

Lakini licha ya kuwa zimebakia siku 2 tu kufika tarehe ya mashindano hayo bado chama hicho kinahitaji msukumo kwa kusaidiwa baadhi ya mahitaji yao yaliobakia ikiwemo fedha za usafiri.

Hassan Haji Silima ambae ni mwenyekiti wa chama hicho alizungumza na mtandao huu na kuelezea mashindano hayo pamoja na mahitaji yao yaliosalia.

“ Kama unavojua tulipokea mualiko kwa wenzetu kutoka Tanzania Bara kushiriki mashindano ya Kilimanjaro Marathon, lakini bado tunahitaji kusaidiwa nauli za usafiri kutoka Zanzibar kwenda Dar-es-salam na kutoka Dar-es-salam kurudi Zanzibar, mana mambo mengine tayari tushapata wasaidizi na vijana wao wenyewe wamepania kwenda kushiriki kwasababu gharama nyengine watajitolea wenyewe, hivyo kama kuna mtu anaouwezo aje atusaidie”. Alisema Silima.

Mashindano hayo ya Kilimanjaro Marathon kwa wana michezo wenye ulemavu wa viungo Tanzania yataanza tarehe 27 ya mwezi huu wa pili 2016 ambapo Zanzibar wanatarajia kuondoka tarehe kesho tarehe 26 kwa jumla ya msafara wa watu 10 wakiwemo viongozi 3 na washiriki 7.

Donald Ngoma Kuwakosa Mabingwa Wa Mauritius Jumamosi
Wachezaji Wa Coastal Union Wawasha Moto Klabuni