Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imepokea fomu za mgombea Urais kupitia chama cha mapinduzi CCM na kumpitisha kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba 28,2020

Mwenyekit wa NEC Semistocle Kaijage amesema Tume imewapitisha wagombea hao baada ya kujiridhisha wamekidhi matakwa ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dokta Wilson Mahera Mkurugenzi wa uchaguzi NEC ametaja vigezo ambavyo vimepelekea wagombea hao kupitishwa na NEC katika kugombea kiti cha Urais.

  • Wagombea wametoa taarifa kuwa wana sifa za kugombea,
  • Katibu mkuu wa chama ametoa uthibitisho wa kuwateua wagombea,
  • Wagombea wamedhaminiwa na wapiga kura kutoka katik mikoa 10iliyokuwa inatakiwa na 5 ya ziada na mikoa 2 ya zanzibar pia wanayo naya ziada.
  • sifa zingine ni Wasimamizi wa uchaguzi wamethibitisha majina ya wadhamini,
  • Wagombea wametoa tamko mbele ya jaji wa mahakama kuu kuthibitisha kwamba wanazo sifa za kuteuliwa,
  • Wagombea wamewsilisha stakabadhi ya shilingi milioni moja .
  • Wagombea wamewasilisha nakala nne za picha ya kila mgombea,
  • Wagombea wametoa tamko la kutekeleza na kuheshimu maadili ya uchaguzi ya mwaka 2020.

Hali kadhalika naye Profesa Ibrahim Lipumba amepitishwa na (NEC) Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Hamida Abdallah Huweishi, kuwa mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais kupitia chama cha CUF.

Wengine waliopitishwa ni Leopard Mahona wa (NRA), John Shibuda wa (Ada Tadea), Mutamwega Mgaiwa wa (SUA) na Cecilia Mwanga wa Demokrasia Makini.

Zoezi la uchukuaji na urudishaji fomu lilianza Agosti 5, 2020 na kukamilika leo agosti 25, 2020.

Kaze, Yacouba kuwasili Dar juma hili
Azam FC Waboresha mikataba benchi la ufundi