Timu ya Taifa ya soka ya Vijana chini ya miaka 15, kesho itaanza rasmi ziara ya mkoani Morogoro ambako watakuwa na mchezo wa kirafiki kesho jioni na keshokutwa asubuhi.

Vijana hao 22, waliopo kambini kujiandaa Dar es Salaam wanajiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Shelisheli unaotarajiwa kufanyika Desemba 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo huo ambao una baraka za Shirikisho la Kimataifa la soka duniani FIFA, umepangwa kufuata taratibu zote za kimataifa ikiwa ni pamoja na kupigiwa Nyimbo za Taifa kwa timu zote sambamba na kupandisha Bendera za Mataifa husika.

Mara baada ya Morogoro itakayofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, timu hiyo itarejea Dar es Salaam jioni ya Desemba 9, 2016 kujiandaa na safari ya Zanzibar Desemba 11 ambako itakuwa na michezo miwili mingine ya kirafiki.

Zanzibar itacheza na Kombaini ya timu ya Vijana wa Zanzibar Desemba 12, 2016 kabla ya kurudiana Desemba 14, mwaka huu na timu hiyo na Kombaini kabla ya kurejea Bara Desemba 15, kujiandaa na mchezo kirafiki wa kimataifa dhidi ya Shelisheli.

Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu wa timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 14, Oscar Mirambo anayepata ushauri kutoka kwa Mshauri Mkuu wa Maendeleo ya Soka la Vijana, Kim Poulsen kinaundwa na makipa ni Shaban Hassan Kimwaga na Abdulatif Noor Lema.

Walinzi ni Kareem Bakari Mfaume, Asante Hamis Bwatam, Rashid Hamisi Rashid, Moris Michael Njako, Harubu Juma Tanu, Cosmas Lucas Jakomanya, Salim Abubakar Lupepo na Dastan Daniel Matheo.

Viungo ni Edson Jeremiah Mshirakandi, Jonathan Raphael Kombo, Alphonce Mabula Msanga, Erick Boniface Bunyaga, Gssper Godfrey Gombanila, Sabri Dahari Kondo na washambuliaji ni Jafari Juma Rashid, Ludaki Juma  Chasambi, Steven Emmanuel Sodike, Michael Mussa Mpubusa na Edmund Geofray John.

Timu hii inaundwa na vijana ambao TFF iliwakusanya tangu 2014 na kuwaunganisha kwa pamoja katika Shule ya Msingi na Sekondari ya Kukuza Vipaji ya Alliance iliyopo Mwanza. Mbali ya kutoa elimu ya msingi na sekondari, pia Alliance inatoa elimu ya awali kwa watoto wa kuanzia umri wa miaka miwili hadi sita.

Timu hii inaandaliwa kuja kwa time mpya ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ambao watashiriki fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa vijana mwaka 2019 ambako Tanzania imeteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuwa mwenyeji. Kambi itavunjwa Desemba 18, mwaka huu.

Meya wa Chadema aeleza kwanini hawakushiriki ziara ya Makonda
Aadhibiwa Kwa Kuidanganya Kamati Ya Saa 72