Mwili wa Msanii wa vichekesho Amri Athumani ‘ maarufu kama King Majuto’ aliyefariki Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu kuagwa leo katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Rais wa shirikisho la filamu Tanzania, Simon Mwakifamba amesema, Mzee Majuto ataagwa saa nane mchana katika viwanja vya Kamrijee na saa kumi Jioni atasafirishwa kwenda nyumbani kwake Tanga kwa mazishi.

“Taarifa hii tumewasiliana na familia nikwamba, Mzee Majuto ndugu jamaa na marafiki watatoa heshima za mwisho na baada ya hapo mwili utapelekwa nyumbani kwake Tanga kwa ajili ya mazishi” amesema Simon Mwakifamba.

Mtoto wa Mzee Majuto, Ashrafu amesema ratiba kamili ya mwili wa Mzee Majuto ni kwamba asubuhi mwili utaoshwa katika Hospitali ya Muhimbili na shughuli zote ndogo ndogo zitafanyika hapo na baada ya hapo mwili utapelekwa kiwanja cha Karimjee kwa ajili ya kuagwa saa nane mchana, na saa kumi mwili utasafirishwa Tanga kwa ajili ya kuzikwa”

Ashrafu aliendelea kusema kuwa Mzee Majuto alipelekwa hospitalini ya Muhimbili Julai 31 baada ya hali yake kubadilika.

“Hali yake ilibadilika majira ya saa tisa alasiri ya leo hivyo kuhamishwa kutoka jengo la Sewahaji kwenda ICU. Ilipofika saa 1.30 jioni hii hali yake ilibadilika zaidi na madaktari walijitahidi kuokoa maisha yale bila mafanikio. Ilipofika saa 2 usiku akafariki,”

Amri Athuman’ King Majuto’ alizaliwa mwaka 1948 jijini Tanga na kusoma shule Msambwini, Tanga, alianza kuigiza 1958 akiwa na umri wa miaka 9 akiigiza katika majukwaa.

Mzee Majuto ambaye alikuwa mtunzi, muigizaji, mwandishi wa mswada na pia ndiye muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company ( TFC).

Ousmane Dembele aikana Arsenal
JPM atuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha 'King Majuto'