Harakati za kuwania nafasi ya kucheza fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 zitakazofanyika nchini Urusi, ziliendelea tena alfajiri ya hii leo kwa michezo mitano ya ukanda wa kusini mwa bara la Amerika (CONMEBOL).

Mabingwa wa kihistoria Brazil, walicheza katika uwanja wa nyumbani wa Arena Amazonia uliopo mjini Manaus dhidi ya Colombia ambao walikubali kisago cha mabao mawili kwa moja.

Mabao ya Brazil katika mchezo huo yalifungwa na Miranda pamoja na Neymar katika dakika ya 2 na 74, huku bao la Colombia likifungwa na Marquinhos aliejifiunga mwenyewe dakika ya 36.

Kwa upande wa timu ya taifa ya Argentina ambayo ilicheza nyumbani dhidi ya Venezuela, walikubali kubanwa kwa kulazimishwa sare ya mabao mawili kwa mawili .

Venezuela walianza kufunga mabao mawili ya kuongoza katika dakika ya 35 na 53 yaliyofungwa na Anor na Martinez, lakini Argentina walijibu mabipo kwa kusawazisha kupitia kwa Prattor na Otamendi katika dakika ya 58 na 83.

Uruguay, wakiwa nyumbani kwao walichomoza na ushindi wa mabao manne kwa sifuru dhidi ya Paraguay, ambapo wafungaji walikua Rodriguez, Luis Suarez pamoja na Edinson Cavani aliyefunga mabao mawili.

Michezo mingine ya ukanda wa CONMEBOL iliyochezwa leo alfajiri,

Chile 0 -0 Bolivia

Peru 2 -1 Ecuador

Mpaka sasa msimamo wa kundi la CONMEBOL unaonekana hivi.

SAMERICA-TEBO-SEP7

CONMEBOL itatoa nchi 4 kutinga fainali za kombe la dunia mwaka 2018.

Nchi hizo zinaweza kuwa 5 ikiwa timu itakayomaliza nafasi ya 5 kwenye kundi lao itashinda mchezo ya mchujo dhidi ya timu nyingine toka bara jingine ambayo itakuwa ni moja toka ukanda ya Oceania wenye nchi za visiwani ambazo ni New Zealand, New Caledonia, Fiji, Papua New Guinea, Solomon Islands na Tahiti.

Eddie Howe Kumbadili Arsene Wenger?
Video: JPM afichua utapeli Magomeni Kota, Amshukuru mzee wa CUF