Rais wa chama cha madaktari Tanzania (MAT), Dkt. Shadrack  Mwaibambe amewataka madaktari wote nchini kuendelee kutoa elimukubwa juu ya ugonjwa wa ebola huku wananchi wakitakiwa kuachana na safari zisizo za lazima ili kuepukana na ugonjwa huo.

Dkt. Mwaibambe amesema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa 54 wa chama hicho uliofanyika jijini Arusha na kuongeza kuwa kutokana na kuwepo kwa mlipuko huo jamii inatakiwa kuelimishwa mapema kuchukua tahadhari ikiwemo  kuepukana na safari zisizo za lazima kwenda nchini Uganda.

“Kumekuwepo na muingiliano mkubwa sana wa wananchi kwenda nchi jirani kwa ajili ya shughuli mbalimbali kwani Uganda hapo sio mbali ni kilometa mia mbili kutoka mpaka wa Tanzania, hivyo ni lazima kila mmoja wetu atoe elimu ya kutosha ili wananchi waweze  kuchukua tahadhari mapema,“ amesema  Dkt. Mwaibambe .

Picha ya pamoja ya madaktari

Amesema kuwa, katika mkutano huo watajadili agenda ya umuhimu wa kupata chanjo ya pili ya uviko19 kwa wale ambao hawakupata awamu ya kwanza sambamba na kujadili  namna ya kuchukua  hatua katika kudhibiti ugonjwa wa Ebola.

Mlipuko wa janga la Ebola umeripotiwa kutokea nchi jirani ya Uganda ambapo kwa taarifa za Septemba 28 vifo vimeendelea kuripotiwa.

 

CAF yapangua ratiba Ligi Kuu Tanzania Bara
Rais Samia awakanya wanaosubiri mkeka