Aliyetobolewa macho na Scorpion, Said Mrisho ameweka wazi juu ya tuhuma zinazomkabili kuhusu kuitelekeza familia yake.

Leo Said amehojiwa na Clouds Media na kukanusha juu ya tuhuma hizo na kudai kuwa hajamtelekeza mke wake bali ameamua kumuacha na kuoa mke mwingine.

Said amesema amechukua uamuzi huo wa kumuacha mke wake kwani  ndoa aliyofunga na mwanamke huyo ilikua ni ndoa iliyoshinikizwa na  wazazi wa upande wa mwanamke ili waweze kurithi mali alizokabidhiwa pindi alipokutwa na matatizo.

Said amekiri kuwa kwa sasa ameoa mwanamke mwingine, ila mke wake ambae ni mama watoto wake amempangia nyumba.

Siku chache zilizopita mke wa Said anayejulikana kwa jina la Stara, alihojiwa na vyombo vya habari na kutoa ushuhuda huo kuwa mume wake Said Mrisho alimpangia njama amtoroke yeye na watoto wake.

“Ni kweli nimeachana na mke wangu ambaye nimefunga nae ndoa hivi karibuni baada ya kupata matatizo, ila sijatelekeza familia, na hii ndoa nimefunga kutokana na shinikizo kutoka kwa wazazi wa mke wangu ili tukiachana tuweze kugawana vifaa vilivyokuja (mali). Japokuwa tumeachana lakini nimempangia nyumba na namsaidia kwasababu nina familia nae. Kwa sasa nimeoa mke mwingine.” amesema Said Mrisho.

 

 

Lowassa alivyotumia dakika 30 makao makuu ya Polisi leo
Rama Dee awaomba msamaha mashabiki, Clouds FM kuhusu ‘Anti-Virus’