Kiungo wa mabingwa wa soka Tanzania bara Simba SC Said Ndemla, amesema amepokea ofa nyingi kutoka kwenye klabu za ligi kuu Tanzania ikiwemo na Young Africans, kutaka kumsajili mwishoni mwa msimu huu.

Mkataba wa Ndemla na klabu ya Simba SC utafikia tamati mwishoni mwa msimu huu, huku wadau wa soka nchini wakimshauri kuondoka klabuni hapo kutokana na changamoto ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza kwa muda mrefu.

Kiungo huyo mwenye sifa ya kupiga mashuti ya mbali, amesema kwa sasa anasubiria mkataba wake utakapomalizika, ili afanye maamuzi ya wapi anastahili kwenda kucheza soka la ushindani.

“Kwa sasa siwezi kuzungumzia ofa za timu nyingine bali naifikiria kushinda taji la ligi kuu Tanzania Bara na taji la shirikisho (ASFC) nikiwa na Simba, ndio malengo yangu kwa sasa.

“Natamani kucheza soka nje ya Tanzania  lakini naamini ipo siku nitafanikisha ndoto zangu kwa ujumla, kwa sababu mpira ndo kazi yangu kwenye maisha ya kila siku,” alisema Ndemla.

Prof. Kabudi ataja hatua 12 nchi za SADC kuikabili Corona
Nchi mbili pekee hazijaathirika na Corona Afrika

Comments

comments