Mwimbaji wa muziki wa asili, Saida Karoli ambaye wimbo wake ‘Maria Salome’ umepata mashavu mawili makubwa mwaka huu kwa wakali wa Bongo Fleva, amezungumzia kitendo cha Darassa kuweka vionjo vya wimbo wake huo kwenye wimbo wake mpya bila kuomba ridhaa yake.

Darasa aliachia wimbo ambao sasa ‘watoto wa mjini’ wanauita ‘wimbo wa Taifa wa Bongo Fleva’ alioubatiza jina la ‘Muziki’ ukiwa na vionjo vya ‘Maria Salome’ siku chache baada ya Diamond kuachia ‘Salome’ yenye vionjo hivyo ambavyo yeye aliomba ridhaa kwa uongozi wa Saida Karoli.

Akizungumzia uamuzi huo wa Darassa, Saida Karoli amesema kuwa hana tatizo naye kwakuwa kwa kufanya hivyo amekuza muziki, lakini alitupa lawama zote kwa mtayarishaji wa wimbo huo kwa kutoomba ridhaa ya kutumia vionjo hivyo.

“Siwezi kumfanya chochote Darassa, kwa kuwa hii ni njia ya muziki wetu kukua, unaweza kuonekana una roho mbaya ukikataza watu wasitumie kazi zako ila kufuata taratibu ni vizuri zaidi,” Saida akakaririwa na BT.

Hivi karibuni, Darassa alisema kuwa awali alipanga kumshirikisha Saida Karoli kwenye wimbo huo kuweka vionjo lakini aliahirisha baada ya Diamond kuachia Salome kabla yake.

 

Msaidizi wa Mbowe adaiwa kutoweka kiutata, Chadema na Polisi watofautiana
Magufuli atoboa siri ya kufuta shamrashamra za uhuru mwaka jana, kuruhusu mwaka huu