Mwanamuziki mkonge wa nyimbo za asili, Saida Karoli amedai kwamba miaka 15 iliyopita alikuwa kwenye jela ya muziki kutokana na kufanya kazi na menejimenti iliyomnyima uhuru katika kazi yake, Saida amelaumu kuhusu kusainishwa mikataba asiyo ielewa  kwani mikataba hiyo ilitumia lugha ngumu ya kiswahili na kingereza huku mwanamuziki huyu akiwa hajui kusoma na kuandika.

Saida amesema kuwa, ”Ile mikataba ilikuwa ya ajabu maana nilingizwa kwenye mikataba iliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza na kiswahili cha ndani ambapo mimi sikuwa nikijua kusoma wala kuandika, pia nilikosa uhuru wa mawazo yangu na mambo mengine ambayo kwa sasa nina uhuru, ndiyo maana kuelekea  miaka 15 tangu kuanza muziki najiona kama nilikuwa jela kwa miaka yote 15”.

Saida amesema alikuwa katika kifungo ambacho kilimnyima uhuru wa kupiga hatua ya kujitangaza kimuziki kwani baadhi ya mikataba aliyosainishwa iliminya uhuru hata wa kuzungumza na vyombo vya habari.

Kwa sasa Saida anatamba na kibao chake cha Orugamba uliopo katika albamu yake yenye nyimbo 17, ameeleza pia hivi karibuni atatoa wimbo wake mpya aliyomshirikisha Abelenego Damiani maarufu kama Belle 9, ambaye anatamba na kibao chake cha ‘give to me’

 

Prof. Mwamfupe ateuliwa kuwa Diwani
Mwigulu ang'aka, atishia kuzifuta taasisi zinazotetea mimba na ushoga