Spika wa Bunge, Job Ndugai amepewa siku 14 kuwasilisha utetezi juu ya madai yaliyofunguliwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe juu ya mamlaka ya kikatiba ya kumuita Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali nchini (CAG) Profesa Mussa Assad.

Uamuzi huo umetolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania, wakati ikisikiliza kwa mara ya kwanza kesi hiyo ya Kikatiba iliyofunguliwa na Zitto Kabwe ambapo mahakama imepanga kuisikiliza rasmi Februari 15.

Aidha, katika kesi hiyo, Zitto Kabwe kupitia wakili wake Fatma Karume atatoa hoja zake na wadaiwa ambao ni Ndugai na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), watatoa utetezi wao kwa kujibu hoja hizo.

Hata hivyo, shauri hilo linasilikizwa na Majaji watatu, Firmin Matogolo, Benhajj Masoud na Elinaza Luvanda ilitajwa ambapo hapo jana kupitia Wakili wa Serikali, Alesia Mbuya aliomba kuongezewa muda wa kuwasilisha maombi hayo.

Mahakama yawaachia huru watuhumiwa wa ugaidi Kenya
Serikali kuongeza nguvu sekta binafsi

Comments

comments