Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Zambia Clatous Chotta Chama amelazimika kuweka wazi mustakabali wake baada ya kuwapo mgongano wa mawazo kati yake na wakala wake ambaye anahitaji kuona anajiunga na Young Africans endapo ataondoka kwa mkopo RS Berkane ya Morocco.

Taarifa zinaeleza kuwa, baada ya Chama kuwa na wakati mgumu huko Morocco, anajipanga kuvunja mkataba na Waarabu hao na chaguo lake la kwanza ni kurejea Simba SC licha ya ofa nono inayotaka kutolewa na Young Africans.

Mapema juma hili kumekuwa na tetesi mbalimbali za usajili huku Chama akihusishwa na kutua Young Africans na Aucho akitajwa kuwa mbioni kuondoka katika klabu hiyo katika kipindi cha dirisha dogo la usajili kinachotarajiwa kufunguliwa Desemba 15, mwaka huu.

Na Young Afrcans imetoa kauli hiyo ikiwa ni siku mbili tu zimepita baada ya kuanguka katika kesi ya kimkataba waliyofungua katika Mahakama ya Usuluhishi ya Masuala ya Michezo (CAS), dhidi ya mchezaji wao wa zamani, Mghana Bernard Morrison ambaye kwa sasa anaichezea Simba SC.

Young Africans walimshtaki Morrison katika mahakama hiyo kwa kuvunja mkataba na klabu hiyo, lakini CAS imetoa hukumu kuwa nyota huyo hakuwa na mkataba na Young Africans baada ya ule wa awali wa miezi sita kumalizika Julai 14, mwaka jana na wanatakiwa kumlipa fidia ya Sh. milioni 12.

Rada za Kocha Pablo zainasa Red Arrows
Young Africans kumuuza Aucho