Shirikisho la Soka nchini Tanzania ‘TFF’ limetoa ufafanuzi wa kuachwa kwa baadhi ya Wachezaji katika Kikosi cha Timu ya Taifa ‘taifa Stars’ ambacho kimeweka Kambi nchini Misri, kwa ajili ya maandalizi ya michezo miwili ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ dhidi ya Uganda.

Taifa Stars itacheza mchezo wa mzunguuko watatu wa Kundi F dhidi ya Uganda kesho Ijumaa (Machi 24) katika Uwanja wa Suez Canal mjini Ismailia-Misri, kabla ya timu hizo kucheza mchezo wa Mzunguuko wanne Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam Machi 28.

Kelele zimekuwa nyingi kwa baadhi ya Mashabiki wa Soka la Tanzania hasa baada ya kuachwa kwa Mabeki wa pembeni wa Simba SC Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na Shomari Kapombe ambao wanadaiwa kuwa na kiwango cha kuitwa katika kikosi cha Taifa Stars kwa sasa.

Kutokana na malalamiko hayo kuzidi kuchukuwa nafasi kubwa katika Mitandao ya kijamii  na baadhi ya vyombo vya Habari, Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao amesema Shirikisho halina mamlaka yoyote ya kutengua maamuzi ya Benchi la Ufundi la Taifa Stars, hivyo maamuzi ya uteuzi wa kikosi ya Kocha Adel Amrouche watayaheshimu.

“Mwalimu ndiye aliyepewa mamlaka ya kuchagua kikosi cha Taifa Stars kwa Asilimia Mia. Hili ni jambo lake.Niliona mitandaoni watu wakilalamika na kuhoji. Mwalimu alikuwa anafanya kazi yake muda tu, ndiyo maana mliona tukachelewa kumtangaza. Hii ni timu ya watu wote”

“Mwalimu hawezi kumuacha mchezaji moja kwa moja. Kazi yetu TFF kumsaidia mwalimu katika mambo ya kiutawala. TFF hatuwezi kumuingilia mwalimu. Kila mmoja anafanya katika majukumu yake ya kila siku. Mimi ni kocha pia, siwezi kukubali kuingiliwa na watu, hivyo hata mimi siwezi kuona mwalimu anaingiliwa.” Amesema Katibu Mkuu wa TFF

Kikosi kilichotajwa na Kocha Adel Amrouche na tayari kipo kambini upande wa Walinda Lango ni Aishi Manula (Simba), Beno Kakolanya (Simba), Metacha Mnata (Yanga), Kibwana Shomari (Yanga), Datius Peter (Kagera Sugar), Yahya Mbegu (Ihefu), David Luhende (Kagera Sugar) Dickson Job (Yanga), na Abdallah Mfuko (Kagera Sugar)

Wengine ni Bakari Mwamnyeto (Yanga), Ibrahim Baka (Yanga), Mudathiri Yahya (Yanga), Sospeter Bajana (Azam FC), Mzamiru Yassin (Simba), Yusuph Kagoma (Singida BS) na Ramadhani Makame (Bodrumspor-Uturuki).

Pia wamo Abdul Suleiman (Azam FC), Edmund Joh (Geita Gold), Fisal Salum (Yanga), Khalid Habibu (KMKM FC), Anuary Jabiri (Kagera Sugar), Simon Msuva (Al-Qadslah-Saudi Arabia), Mbwana Samata (KR Genk-Ubelgiji), Novatus Dismas (Zulte Waregem- Ubelgiji), Alphonce Mabula (FX Spartak Subotica-Serbia), Kelvin John (KRC Genk-Ubelgiji), Ben Starkle (Bastord United FC-Uingereza), Haji Mnoga (Aldershot Towan-Uingereza), Ally Msengi (Swallows-Afrika Kusini), Himid Mao (Ghazi El Mahallah SC- Misri) na Said Khamis (Al-Fujairah-UAE).

Tanzania inatafuta tiketi ya kucheza AFCON 2023 baada ya kushiriki Fainali hizo mara mbili mwaka 980 ilipata nafasi kwa mara ya kwanza katika fainali zilizofanyika nchini Nigeria huku 2019 ikicheza mashindano hayo nchini Misri.

Mahmoud Kahraba amaliza utawala wa Chama
BAKWATA waandamana kupinga ukatili kijinsia, ndoa za utotoni