Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amejibu tuhuma za kutelekeza mtoto, baada ya picha kuzagaa kwenye mitandao ikimuonyesha mtoto ambaye amefanana naye akitajwa kumtelekeza.

Amesema kuwa alichokiandika kwenye mitandao ya kijamii anamaanisha hivyo anamtaka mwanamke huyo ambaye ametajwa kuwa miongoni mwa walioenda kwa mkuu wa mkoa wa Dar e salaam, Paul Makonda kwa kutelekezwa, asiishie hapo tu bali aende hata Bungeni.

“Ilikoanzia imeanzia kwa Jerry Muro ndiye kasambaza hizi habari, kitu ambacho nakijibu hapa amekianzisha Jerry Muro, sasa mimi nasema kama huyo mtu yupo, nimetoa namba zangu na kama sipatikani aje hapa Bungeni,” amesema Msigwa

Hata hivyo, hapo jana Peter Msigwa aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa facebook akisema kwamba iwapo kweli mwanamke huyo yupo na akithibitisha ni kweli amemtelekeza, basi yupo tayari kujiuzulu ubunge wake alionao.

Zuckerberg aliomba radhi bunge la Marekani
Rais awaachia huru wafungwa wote wa kisiasa