Spika wa zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pius Msekwa amesema kuwa Wabunge hawafuati utaratibu kwa kufanya maamuzi yao binafsi.

Msekwa amesema kuwa kuna taratibu za matibabu kwa Wabunge na hairuhusiwi kutibiwa hospitali yoyote kwa uamuzi binafsi lakini wanashindwa kufuata miongozo hiyo na kuibua migogoro.

“Mbunge akiugua huwa anapelekwa hospitali ya serikali na endapo akitakiwa kuhamishwa hospitali atapewa rufaa na lazima bunge liwe na taarifa hakuna anayefanya maamuzi yake binafsi alafu anahitaji kulipwa,”amesema Msekwa

Amesema kuwa hakuna upendeleo kama ambavyo Kambi ya Upinzani Bungeni inavyodai na imekuwa hivyo tangu mwanzo kwa kuwa fedha zinazotumika ni za umma na zinataratibu zake.

Hata hivyo, ameongeza kuwa si busara kwa wabunge wa upinzani kuzusha kuwa hawapewi kipaumbele pindi wanapougua.

Ngasa arejea nyumbani 'Yanga'
JPM mgeni rasmi siku ya mazingira duniani