Mpango wa klabu ya Everton kusaka meneja atakaerithi, nafasi ya Roberto Martinez umeanza kuonyesha muelekeo, kufuatia hoja ya Ronald Koeman kuwa chaguo la wengi kupata nguvu.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake makuu mjini Liverpool nchini England, zinaeleza kwamba, hoja ya kuajiriwa kwa meneja huyo kutoka Uholanzi imepewa kipaumbele kikubwa na huenda wakakamilisha suala la kumuajiri mapema juma lijalo.

Mfanyabiashara kutoka nchini Iran ambaye ana asilimia kubwa ya hisa ndani ya klabu ya Everton, Farhad Moshiri amekua mstari wa mbele kuona Ronald Koeman anaajiriwa klabuni hapo kutokana na kuifahamu vyema ligi ya nchini England, tofauti na majina ya mameneja wengine wanaopendekezwa.

Hata hivyo, mkakati wa Everton kumpa ajira Koeman utakabiliwa na changamoto ya kuvunjwa kwa mkataba wa meneja huyo ambaye kwa sasa ni mfanyakazi wa klabu ya Southampton.

Kwa upande wa Koeman, mwenye umri wa miaka 53, ameshaanza kuonyesha viashiria vya kuachana na klabu ya Southampton, baada ya kuieleza familia yake kuhusu kubadili mazingira ya kazi yake kwa sasa.

Mmoja wa watu wa familia ya Koeman, amesema baba yao aliwaeleza jambo hilo katikati ya juma lililopita baada ya kurejea nyumbani kwao Uholanzi kwa mapumziko.

EUnai Emery

Wakati mkakati huo ukiendelea kufanywa, meneja wa mabingwa wa Europa league Sevilla CF, Unai Emery ameweka kama mbadala wa Koeman endapo mambo yatakwenda tofauti na inavyotarajiwa.

Elias Maguri Afikiria Kurudi Msimbazi
Abdallah Ahmed Bin Kleb Awatosa Kiaina Kina Manji